Mwezi Desemba 2024, GASCO iliingia mkataba na PUMA kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi linalounganisha na vituo vya PUMA CNG vinavyojengwa katika maeneo ya Mbezi Beach Tangibovu na Tegeta IPTL. Ujenzi wa bomba la gesi la inchi 4 kuelekea Kituo Kikuu cha PUMA CNG kilichopo Tegeta upo katika hatua za mwisho, huku mtandao wa bomba uliotekelezwa katika Kituo cha PUMA Bagamoyo Road CNG ukiwa umekamilika kwa mafanikio.
GASCO inatekeleza kazi hizi za ujenzi wa mabomba ya gesi kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora, usalama, na kufuata kikamilifu viwango vya kimataifa.
Hadi sasa, mradi umefikia asilimia 81.28%, huku ununuzi wa vifaa muhimu vya muda mrefu (FMS na Odorization skids) ukiendelea kwa ajili ya Kituo Kikuu cha PUMA CNG Tegeta. Mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Septemba 2025
Mradi umefikia asilimia 78% kwa sasa - manunuzi ya FMS na Odorisation Skid yanaendelea kwa sasa
Kuanza rasmi kazi za mradi
Kusaini mkataba wa makubaliano na PUMA Energies