GASCO imepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 ya utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kuendesha na kujenga miundombinu ya gesi asilia:
- Uendeshaji na Matengenezo (O&M): GASCO inasimamia kwa ufanisi mkubwa uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya gesi asilia, na kufikisha miaka 10 ya uendeshaji bila ajali kazini (Zero LTI) ishara ya usimamizi salama na wenye viwango.
- Huduma kwa Wateja: Katika kipindi chote, imehakikisha gesi asilia inapatikana kwa uhakika kwa wateja wa majumbani, taasisi na viwanda.
- Ujenzi wa Miundombinu ya Gesi Majumbani: GASCO imetekeleza miradi ya ujenzi wa usambazaji gesi asilia majumbani kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi, na Dar es Salaam kwa matumizi ya kupikia.
- Kuunganisha Taasisi za Elimu: GASCO imetekeleza miradi ya ujenzi wa usambazaji gesi asilia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu (DUCE).
- Vituo vya Gesi Iliyoshindiliwa (CNG): GASCO imetekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha vituo vya kujazia gesi asilia iliyoshindiliwa kwenye magari, vilivyopo Tangi bovu, Tegeta, Goba, Mwenge Cocacola na Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam.
- Kuunganisha Viwanda na Mitambo ya Umeme: GASCO ametekeleza ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha gesi asilia viwandani na kwenye mitambo ya kuzalisha umeme.
- GASCO imepata kandarasi ya uendeshaji na matengenezo ya kituo cha TPDC CNG cha Mlimani.