Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Nishati

Gas Company (Tanzania) Limited

Usafirishaji wa Gesi

Imewekwa: 11 January, 2023
Usafirishaji wa Gesi

GASCO inaendesha na kusimamia bomba la kusafirisha gesi asilia la mgandamizo wa juu lenye umbali wa KM 551 kutoka Madimba Mtwara na Songosongo Lindi hadi Tegeta Dar es Salaam. Bomba hili linajumuisha vituo vikubwa vitatu (kituo cha kuunganishia gesi Somanga, kituo cha kupokelea gesi Kinyerezi na kituo cha Tegeta) na jumla ya vituo vidogo vya valvu 16. Bomba hili lina uwezo wa kusafirisha gesi hadi futi za ujazo milioni 784 mmscfd bila mgandamizo na futi za ujazo milioni 1002 mmscfd baada ya mgandamizo. Bomba hili lilianza kufanya kazi mnamo Oktoba 2015 na kwa sasa linasafirisha gesi kwa wastani wa futi za ujazo milioni 140 mmscfd. Idara ya usafirishaji wa gesi inajihusisha na usimamizi na matengenezo ya miundombinu ya bomba la gesi, uthibiti wa miundombinu ya bomba dhidi ya mmomonyoko na shughuli zingine za kibinadamu ambazo zinaweza kuathiri ubora wa miundombinu ya bomba.