Mradi huu unahusisha utekelezaji wa kazi za Uhandisi, Ununuzi wa vifaa, na Ujenzi (EPC) kwa ajili ya uunganishaji wa miundombinu ya gesi asilia kwenye Kituo cha Kujaza Gesi Asilia (CNG) cha TANHealth kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam. Mkataba wa utekelezaji wa mradi ulisainiwa tarehe 20 Februari 2025, kwa muda wa miezi minne, na kazi za awali zilianza rasmi kwenye eneo la mradi tarehe 28 Juni 2025.
Mradi umefikia hatua ya utekelezaji wa asilimia 54.15%, ambapo shughuli za ununuzi wa kifaa kikuu cha mfumo wa upokeaji gesi (FMS skid) bado zinaendelea. Kukamilika kwa mradi kunatarajiwa kufikia tarehe 30 Septemba 2025. Mradi huu ni sehemu ya juhudi za GASCO za kupanua matumizi ya gesi asilia iliyoshinikizwa (CNG) kwa ajili ya usafirishaji na matumizi mengine rafiki kwa mazingira.
Mradi unaendelea na umefikia asilimia 54.15%
Kuanza rasmi kazi za Mradi
Kusaini Mkataba