Mha. Baltazari T. Mrosso

Wasifu
Karibu GASCO (Gas Company (T) Limited)
Mimi, kama Meneja Mkuu wa GASCO, ninayo furaha kubwa kukukaribisha rasmi kupitia tovuti yetu.
GASCO imejikita katika kuhakikisha uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya kitaifa ya gesi asilia nchini Tanzania kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu. Tunahudumia vituo vya uchakataji gesi, mabomba ya usafirishaji na usambazaji gesi asilia, pamoja na miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha gesi kwa wateja.
Tumejidhatiti katika kuhakikisha usalama, uendelevu, na ubora kwa kiwango cha juu, huku tukihakikisha upatikanaji wa huduma za gesi kwa uhakika sambamba na kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa pamoja na ubunifu.
Tunathamini sana imani na ushirikiano wa wadau wetu wote wakiwemo wateja, washirika, wafanyakazi na jamii kwa ujumla. Uhusiano wa pamoja, uwazi, na uadilifu ndiyo msingi wa njia yetu ya kufanya kazi.
Kadri tunavyokabiliana na changamoto za sekta ya nishati, GASCO itaendelea kujikita katika kuchangia kwa dhati katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia usimamizi bora na wa uwajibikaji wa rasilimali za gesi asilia.
Karibu udhuru tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu huduma, miradi na dhamira ya GASCO ya ubora.