Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Nishati

Gas Company (Tanzania) Limited

"Pigging", zoezi la kuingiza kifaa maalum kinachoitwa "pig" ndani ya bomba la gesi

Imewekwa: 29 July, 2025
"Pigging", zoezi la kuingiza kifaa maalum kinachoitwa "pig" ndani ya bomba la gesi

Pigging ni zoezi la kuingiza kifaa maalum kinachoitwa "pig" ndani ya bomba la gesi kwa ajili ya kusafisha, kukagua au kutathmini hali ya ndani ya bomba bila kusimamisha shughuli za usafirishaji wa gesi.

Kampuni ya GASCO inaendesha zoezi maalum la pigging katika bomba kuu la gesi asilia linalotoka Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) kuelekea Dar es Salaam. Hadi sasa, kipande cha kwanza cha pig tayari kimepokelewa katika Kituo cha Somanga Fungu, hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa bomba linaendelea kusafirisha gesi kwa ufanisi, usalama na kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.