Uendeshaji wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia kwa Vyombo vya Moto (CNG)
Uendeshaji wa Vituo vya Kujaza Gesi Asilia kwa Vyombo vya Moto (CNG)
Imewekwa: 29 July, 2025

Kituo cha CNG cha TPDC kinasimamiwa na kuendeshwa na Kampuni ya GASCO kwa lengo la kuhakikisha huduma ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) inapatikana kwa ubora wa hali ya juu, sambamba na kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa. Kampuni pia inahusika na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia, vituo vya kujazia gesi iliyoshindiliwa (CNG) kwa magari, pamoja na vituo vya mafuta vinavyotoa huduma ya gesi.