GASCO Yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani – 5 Juni 2025
GASCO Yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani – 5 Juni 2025
Imewekwa: 28 July, 2025

GASCO imeshiriki kikamilifu katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni 2025, chini ya uongozi wa Meneja Mkuu Mhandisi Baltzar T. Mrosso. Maadhimisho haya yalihusisha zoezi la upandaji miti, likiwashirikisha watumishi kutoka idara mbalimbali kama sehemu ya juhudi za kulinda na kuhifadhi mazingira.
Kupitia zoezi hilo, GASCO imedhihirisha dhamira yake ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuchangia katika jitihada za taifa na dunia nzima katika kulinda mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho. Izingatiwe kuwa kampuni inajihusisha na uendeshaji wa miundombinu ya gesi asilia—nishati safi na rafiki kwa mazingira—hivyo mchango wake unalenga kuendeleza matumizi ya nishati mbadala na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi