Uunganishaji wa ndani kuelekea kiwanda cha Knauf - Mkuranga
Uunganishaji wa ndani kuelekea kiwanda cha Knauf - Mkuranga
Imewekwa: 31 July, 2025

Mradi huu ulitekelezwa baada ya kusainiwa kwa mkataba tarehe 21 Machi 2025, ukiwa na muda wa utekelezaji wa miezi mitatu. Lengo kuu la mradi lilikuwa kufanya kazi za uunganishaji wa ndani wa miundombinu ya gesi asilia kuelekea kiwanda cha Knauf kilichopo Mkuranga. Mradi ulikamilika kwa mafanikio tarehe 22 Juni 2025 na ulikabidhiwa rasmi kwa mteja tarehe 8 Julai 2025. GASCO ilitekeleza kazi hii kwa weledi wa hali ya juu, ikizingatia viwango vya kiufundi na usalama.